Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Ishara ni kubwa, lakini Yezebeli hatubu, bali anataka kumwua Eliya. Hata huyu nabii hodari aliogopa kufa akatoroka. Baadaye alikata tamaa kabisa na kuomba afe. Lililo kubwa ni kwamba Mungu hakumlaumu Eliya wala hakumwacha, bali alimjia na kumlisha na kumwongoza njia aende mlima Horebu, umbali wa km 480 hivi. Wewe Mkristo, ujipe moyo kumweleza Mungu hali yako, hata kama umekata tamaa kabisa. Hakika Mungu atakujibu wewe pia na kukulisha ili uwe na nguvu ya kutosha kwa njia ngumu aliyokupangia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/