Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Mzee mmoja wa baraza alikuwa ameguswa na matendo makuu yaliyotendwa na mitume. Akashauri wasiwazuie mitume wasije wakapingana na Mungu. Akawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu(m.38-39). Je, msomaji, unapinga uamsho ulioletwa na Mungu siku hizi? Ni kweli kwamba kuna aina ya uamsho uliopotoka. Lakini uamsho wa kweli unaovunja nguvu ya dhambi katika maisha yetu na kumtukuza Yesu na damu yake tusiupinge, tusije tukapingana na Mungu!Hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo(m.42).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/