Kuomboleza VyemaMfano
Msiba unapotokea, wengi wanaweza kujiuliza ikiwa Mungu ni mwema au la. Wakati Bwana anapomchukua mtu tunayempenda nyumbani ghafla, inaweza kuonekana kana kwamba Mungu anayo ubinafsi. Watu wengi wametanga mbali na imani kwa sababu wanasikia wakristo wakihubiri kuhusu Mungu mwema ambaye huwachukua wale tunaowapenda kutoka kwetu bila maelezo.
Kujibu hilo, ningesema kwanza, ukimwondosha Mungu, bado una shida yako. Bado kuna magonjwa na uovu. Nafikiri juu ya swali la Yesu kwa Petro katika Yohana 6:67 – 68. Anasema, “Je, utaniacha? Na jibu la Petro ni, “Tungeenda kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.” Jambo ni kwamba hujatatua tatizo lako kwa kumkimbia au kumkana Mungu.
Pili, umewahi kuona kwamba kawaida tunahoji tu wema wa Mungu pale mambo mabaya yanapotokea? Tunakubali wema wake katika nyakati nzuri, lakini tunakataa wema wake wakati mambo yanapoharibika. Tunapaswa kuangalia na kuuweka ubaya wa hali dhidi ya historia ya wema wa Mungu.
Tatu, tunafikia swali hilo la zamani: kwa nini tuna maumivu haya yote, na kwa nini Mungu mwema aruhusu uovu? Mungu amewapa wanadamu chaguo. Pamoja na chaguo hilo huja uwezekano wa matokeo mema na mabaya. Uhuru unaruhusu uovu kuwepo, lakini tunafanya uovu kutokea. Ndiyo sababu tunamhitaji Mungu mwenye enzi na ukuu, anayeweza kuingilia kati hali yetu na kuleta mema kutoka kwa mabaya. Yeye ndiye anayetawala hata wakati mambo katika maisha yako yanaweza kuwa yametoka nje ya udhibiti wako.
SALA: Bwana, ninakuchagua wewe na njia zako juu ya njia za wanadamu. Ninakubali kwamba wewe ndiwe unayetawala licha ya maisha kujawa yote, mabaya na mema, Unaweza kufanya mambo hayo yote pamoja kwa manufaa makubwa zaidi. Nisaidie kuamini ukweli huu kabisa. Ninachagua kukuamini bila kujali maumivu ninayokumbana nayo. Katika jina la Kristo, amina.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana na jinsi alivyompoteza kwa ghafla mpwa wake wa kike. Kanuni hizi zinaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kuomboleza vyema na kukumbatia uponyaji.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative