Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuomboleza VyemaMfano

Kuomboleza Vyema

SIKU 4 YA 6

Huzuni huja kwa kila mmoja wetu kwa njia tofauti. Sio kila mtu huhuzunika kwa njia ile ile. Wengine huhuzunika kwa muda mrefu zaidi. Wengine hawafikii tumaini ambalo Mungu hutoa bila kupitia bonde au msimu mgumu. Baadhi yenu mko katika hali ya hasira kuhusu jambo ambalo limeruhusiwa kutokea katika maisha yako. Hauko peke yako.

Huenda ukawa unasema, “Si sawa,” au “Nina hasira.” Kwanza kabisa, Mungu anaruhusu hasira. Huhitaji kujisikia mwenye hatia kwa sababu umemkasirikia Mungu. Sura tatu za kitabu cha Habakuki ni maneno ya mtu aliyekatishwa tamaa na mwenye hasira. “Mungu unawezaje kuruhusu hili?” Ninaombacho tu ni kwamba, utumie hasira yako kwa heshima. Tayari Mungu anajua jinsi unavyohisi, kwa hivyo kuificha hakufanyi itoweke.

Pia, lazima uwe na theolojia sahihi kuhusu mauti ikiwa utaomboleza vyema. Na kwa kuomboleza vyema, inamaanisha kuomboleza kwa namna ambayo unamheshimu yule uliyempoteza huku pia ukijiruhusu wewe na wale walio karibu nawe kupona na kusonga mbele. Ikiwa huna theolojia sahihi ya kifo, wewe, utaona kifo kuwa ya kudhuru tu. Hata hivyo katika uchumi wa Mungu, kuna auli anayotoa ya kushangaza.

Anasema, "Ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake" (Zaburi 116:15).

Paulo pia asema katika Wafilipi 1:23, “Lakini nimebanwa na pande zote mbili, nikiwa na nia ya kuondoka nikae pamoja na Kristo, maana hilo ndilo bora zaidi.” Lazima uwe na mtazamo wa umilele. Tukikumbuka hilo huku tukionyesha unyoofu wetu kwa Mungu, tukisalia na picha kubwa inayofaa katika maumivu yetu na machozi.

SALA: Baba, ninaamini kwamba una nia mema kwa ajili yangu moyoni mwako hata katikati ya msiba huu mzito. Hata wakati ambapo sielewi kwa nini unaruhusu hasara kama hiyo kutokea, ninajikabidhi kwako na kwa mapenzi yako kamilifu. Nijaze kwa hekima yako, ili niweze kujibia vyema zaidi hasara niliyopata na niinuke juu ya maumivu yangu hadi mahali pa uponyaji na urejesho. Katika jina la Kristo, amina.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Kuomboleza Vyema

Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana na jinsi alivyompoteza kwa ghafla mpwa wake wa kike. Kanuni hizi zinaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kuomboleza vyema na kukumbatia uponyaji.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative