Kuomboleza VyemaMfano
Unawezaje kuwa na ujasiri katika imani yako ikiwa historia na hali zimekuwa ngumu? Unawezaje kupata imani ya ujasiri, hasa wakati umemwomba Mungu akusaidie, na yeye hafanyi hivyo? Au wakati umepoteza mtu ghafla? Au umepoteza mpendwa uliyemtegemea na kumpenda kwa dhati?
Ikiwa umejionea wema wa Mungu siku za zilizopita wakati wa ugumu, bila shaka hiyo inasaidia. Inakupa ujasiri kwamba yeye anaweza kushughulikia leo yako au kesho yako. Kisha unapaswa kuamini katika kweli hii, kwamba kama yeye anaponya maumivu yako mara moja au la, anajua kile anachofanya, kwa sababu umewahi kuiona hapo awali.
Ni lazima tujikumbushe nyakati ambazo ametutendea, ili tuweze kutembea kwa imani asipotenda au kujibu kwa njia tunayotaka ajibu.Tunajua yeye ni mwema. Tunajua anatupenda. Lakini pia tunajua yeye ni mwenye enzi. Lazima tukumbuke hizo zote tatu kwa wakati mmoja.
Kitovu cha kitabu kizima cha Ayubu inajikita kwenye swali, “Kwa nini wenye haki huteseka?” Kumbukumbu la Torati 29:29 inasema kwamba ana mambo ya siri ambayo ndani yake hajibu swali letu la “kwa nini” ambalo tunatafuta. Hiyo ni haki yake. Lakini unapaswa kuamini kwamba Mungu anajua anachofanya wakati hafanyi kile tunachotaka afanye au tunapotaka afanye. Kwa sababu tuna historia ya kujua kile anachoweza kufanya, tunaweza kujua kile anachoweza kufanya ikiwa anafanya au la.
SALA: Baba, nakuomba unijaze amani yako. Ninajua unafanyia mambo yote kazi kuwa mazuri, kwa wakati wako, lakini nipe uhakika kwamba njia zako kwa kweli ndizo bora kwangu. Na ikiwa ni lazima nivumilie msimu mgumu, nipe nguvu na utulivu ya akili ili kuumaliza, nikiwa na nguvu zaidi kuliko nilivyokuwa hapo awali. Asante kwa utunzaji wako usio na kikomo. Katika jina la Kristo, amina.
Kuhusu Mpango huu
Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana na jinsi alivyompoteza kwa ghafla mpwa wake wa kike. Kanuni hizi zinaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kuomboleza vyema na kukumbatia uponyaji.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative