Kuomboleza VyemaMfano
Unapojilnganisha na watu wengine, unapowaangalia wakiwa katikati mwa msiba wao, au uone jinsi wanavyoomboleza, waweza kufikiri, “Mimi sina imani ya kutosha.” Baadhi ya yale yanayotendeka kwa habari ya msimu huu wa majonzi, inajumuisha, theolojia, imani, ufahamu, maarifa na hekima yako. Lakini mengi pia yanahusiana na utu wako. Kwa mujibu wa kutegemea haya mambo, unaweza kukabiliana na dhoruba hii kwa njia bora au mbaya zaidi kuliko wengine.
Kwa hivyo, utu wako na uzoefu wako unahusiano kwa kiasi gani na uwezo wako wa kushughulikia msiba vyema?
Labda ni mchanganyiko wa mambo. Watu wana hisia tofauti. Wao wanajibia tofauti hali zao tofauti. Mungu amewafanya wengine kuwa wapesi zaidi wa kihisia kwa misiba na magumu, na hiyo inaweza kumaanisha kwamba wanaomboleza kwa kina na zaidi na kwa muda mrefu pia kuliko wengine. Wengine wanaweza kujirudisha nyuma kwa haraka kutoka kwenye mchakato wa kuomboleza haraka aitha kwa sababu wamekusudia zaidi au ni wenye ustahimilivu. Jambo ni hili, kwamba Mungu alitufanya kila mmoja wetu tofauti na mwingine, na ni kawaida kudhani kwamba baadhi watapata mchakato wa kuomboleza kuwa mgumu zaidi kuliko wengine.
Lakini kumbuka imani ni nini. Sio hisia. Imani inaonyeshwa katika harakati zako (Yakobo 2:17). Watu wengi wana imani zaidi ya wanavyofikiri, lakini hisia zao ni kama wingu lilowafunikia kabisa wasijue iwe ni imani au la. Kwa hivyo, usichanganye hizo mbili kwa sababu wakati mwingine zi pamoja na wakati mwingine haziko pamoja. Wakati mwingine unapaswa kumwamini Mungu katika hilo giza totoro. Kuna giza nene sana, basi unapaswa kufanya kama Paulo na Sila walivyofanya. Huna budi kumsifu usiku wa manane ukiwa katika minyororo ya maumivu yako. Njia mojawapo ya kutumia imani ni kumsifu katikati ya maumivu yako. Unaweza usijisikie kumsifu na sifa zako sio lazima zije kwa tabasamu na furaha, lakini unaweza wewe mwenyewe kumsifu Mungu kwa kuthibitisha udhibiti wake, hekima na nguvu hata katikati ya hasara.
SALA: Bwana, kukutafuta si rahisi ninapokuwa na uchungu. Ninachotaka kufanya ni kutambaa niwe kama mpira, kisha nikate tamaa ya maisha. Kwa hivyo, ninakuhitaji zaidi kuliko hapo awali; Nahitaji faraja Yako. Ninahitaji busara yako, ili nipate kupata maana zaidi kutoka katika eneo hili lenye giza ambalo nimejikuta. Mtume Roho wako kama mfariji, na uniruhusu kushughulikia maumivu kama mtoto wa ufalme wa Mungu. Katika jina la Kristo, amina.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana na jinsi alivyompoteza kwa ghafla mpwa wake wa kike. Kanuni hizi zinaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kuomboleza vyema na kukumbatia uponyaji.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative