Siku 21 za KufungaMfano
Unawaza kuhusu kuendelea na kifungo chako ama pengine kuanza tabia mpya za desturi ya kufunga mara kwa mara? Katika mlango huu watu wanawaza kuhgusu iwapo wanafaa kuendelea na kalenda ya kufunga waliyokuwa wakitumia na Mungu anawajibu kupitia Zekaria. Mungu alianzisha ratiba kamili ya vifungo na sherehe tangu wakati wa Musa. Vyote viwili vilikusudiwa kuwakaribia watu wake. Ikiwa nia yako ya kila siku ni kujongea karibu zaidi na Mungu, nyakati zote mbili za kufunga na za karamu zinaweza kuwa takatifu kwa Mungu. Chukua muda kumruhusu Mungu kukuongelesha kuhusu muda wa kifungo chako. Mwulize Mungu akusaidie kutafakari kuhusu njia ambazo kifungo chako kimelainisha moyo wako na kubadilisha jinsi unavyotendea wengine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Anza mwaka mpya kwa kulenga nidhamu ya kiroho ya kufunga. Mpango huu unajumuisha vifungu kadhaa kuhusu kufunga, vingine vinahimiza kutafakari ukaribu na Mungu. Kwa siku 21, utapata somo la Biblia la kila siku, ibada fupi, maswali ya kutafakari, na maombi.
More
We'd like to thank Life.Church for their generosity in providing the structure for the 21 Day Fast reading plan.