Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Leo mtume Paulo anajibu swali linalosema: Maana yake nini Biblia inapoongea juu ya sheria na imani? Kwanza analinganisha sheria ya urithi miongoni mwa wanadamu na taratibu ya Mungu. Kuhusu tohara, je, Ibrahimu alipewa ahadi za Mungu kabla hajatahiriwa? Ndiyo. Maana si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa Ibrahimi imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki (Rum 4:9-10). Kutahiriwa kwake kulikuwa muhuri tu ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa. Tujifunze kwamba ahadi ya Mungu juu ya kuhesabia haki iko kabla ya tendo lolote kutoka kwetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/