Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Kabla Kristo hajatukomboa tulikuwa chini ya mawakili na watunzaji, yaani tulikuwa nje ya Kristo. Lakini hali hiyo haikuendelea. Kulitokea utimilifu wa wakati katika mpango wa Mungu (m.4, Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria). Huo uliwadia alipozaliwa Kristo. Ndio utimilifu huo tunaosherekea wakati wa Krismasi: Yesu alizaliwa ili awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana (m.5). Hali hiyo, maana yake ni kuwa na Roho wa Mwana wa Mungu (m.6), tena ni kuwa mrithi (m.7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/