Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 11 YA 30

Tuendelee kujifunza kazi za torati. Kwanza Paulo anafafanua kuwa andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo. Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa (m.22-23). Sheria inatuonyesha kwamba kwa njia ya matendo hatuwezi kuingia mbinguni wala kupata Roho. Hii inatokana na ukweli kwamba torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani (m.24). Kwa hiyosheria inatusukuma kwenda kwa Kristo mwenye kutuhesabia haki. M.25 unaosesema kwamba iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi, una maana kwamba baada ya kumpokea Kristo, sheria haina haki tena ya kutushtaki, kwa sababu tumeamini. M.27-29 inaunganisha imani na ubatizo ikisema kwamba ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. Tulipewa hayo yote katika ubatizo, na tunayahifadhi kwa njia ya imani. Mungu atusaidie!

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/