Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Paulo alikuwa na shaka juu ya Wagalatia. Ndiyo maana anasema, Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu; laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu (m.19-20).Kwa hiyo anaendelea kuwaonyesha laana ya kuwa chini ya sheria na baraka ya kuendelea katika imani. Anatumia mfano wa wana wawili wa Ibrahimu (Isaka na Ishmaeli) kama tunavyosoma habari zao katika Mwa 21:2 na 8-13. Kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi (m.28), siyo kwa uwezo wa wanadamu. Hii ni jambo la maana. M.30 wasema kwamba waaminio watarithi uzima wa mbinguni, bali walio chini ya sheria hawataurithi: Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Yaani mtume hazungumzii jambo dogo. Zingatia onyo la 5:1 kama linavyowekwa wazi hivi, Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/