Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Mtume Paulo anauliza kuhusu kusudi kuu la torati anaposema, Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi? (m.19a). Jibu lake lasema: Iliingizwa kwa sababu ya makosa ya Wayahudi, hata aje huyo mzao (Kristo) aliyepewa ile ahadi (m.19b-22). Kristo alipokuja alileta agano jipya. Sheria ina kusudi lake, na ahadi ina kusudi lake: Sheria haiwezi kuhuisha, bali andiko (= sheria) limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi (m.22a). Bali ahadi tuliyorithi kutoka kwa Ibrahimu yaweza kuhuisha. Sheria huua, na ahadi huhuisha. Hii ndiyo tofauti kubwa kati yao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/