Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Siku hizi wengi huongea juu ya Roho na juu ya miujiza. Hao hujihesabu kuwa wenye utakatifu maalum. Watu hao husema: Imani ni kitu cha kawaida tu. Ili kupata Roho, kwatakiwa kitu kingine maalum. Bali mtume Paulo anasema kwamba twapokea Roho kwa imani, na Mungu hufanya miujiza kati yetu kwa sisi kusikia kunakotokana na imani. Tujifunze kwamba tusidharau imani, bali tuiheshimu, kwa sababu huleta baraka zote za rohoni (Efe 1:3), kama vile Roho Mtakatifu, miujiza na karama za Roho.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/