BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Sura ya 4: Mzingatie Binti Hekima
Katika sura hii baba anamzungumzia mwanawe mara zingine tatu.
Baba Anazungumza na Mwanawe Mara ya Tano
Mstari wa 1-9: Mwanzoni mwa sura hii baba anawaita wanawe ili kuzungumza nao. Anaonekana kama baba mwenye kujivunia japo mwenye wasiwasi kidogo anayewapongeza maharusi. Anatoa wosia aliopewa na baba yake miaka iliyopita, akimsihi amzingatie Binti Hekima. “Atakupa shada la maua kupendezesha kichwa chako na taji kuu,” anasema. Angalia jinsi baba anavyomzungumzia Binti Hekima kwa watoto wake kwa heshima na kwa namna ya kimahusiano.
Baba Anazungumza na Mwanawe Mara ya Sita
Mstari wa 10-19: Sasa baba na mwanawe wanazungumza kama wanaume. Hakuna maneno ya upole kama vile "thamini," heshimu," au "zingatia." Anatumia mbinu ya kutofautisha ili kuwasilisha hoja yake: kuna njia mbili tu maishani—uovu au haki. Tambua kuwa hakuna chaguo la tatu. Chagua nuru au giza, uhai au mauti; uamuzi ni yako. Kama vile tu katika sura ya 3, baba anatumia maneno dhahiri, yenye ufafanuzi ili kuelezea faida na matokeo ya njia hizi mbili tofauti.
Hotuba ya tatu ya Baba kwa Mwanawe
Mstari wa 20-27: Anapozungumza na mwanawe kwa mara ya saba, baba anaendeleza mazungumzo yaliyotangulia. Baada ya kuchagua njia inayofaa, baba anamtayarisha mwanawe kwa safari. Anasisitiza kuwa kufuata njia hii kutahitaji moyo, macho, masikio, mdomo na miguu yake. Hesabu ni mara ngapi kila kiungo kimetajwa. Kufuata njia hii kunahitaji utumuie kila kitu ulichoumbwa nacho. Maneno haya sio ushauri tu— ni "uhai kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili mzima."
Kitabu cha Mithali kinatufundisha jinsi ya kuishi maisha MAZURI - kutembea katika mwangaza tukiambatana na Binti Hekima. Je, uko tayari kuacha njia zipi ili uchague maisha mazuri?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili