Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Hekima ya MithaliMfano

BibleProject | Hekima ya Mithali

SIKU 10 YA 32

Sura ya 9: Simulizi kuhusu Nyumba Mbili

Binti Hekima Anazungumza kwa Mara ya Nne

Muundo wa sura hii ni wa ulinganifu sana. Unaanza kwa mwaliko wa mistari 6 kwa nyumba ya Binti Hekima (1-6) na inakamilika kwa mwaliko wa mistari 6 kwa nyumba ya mwanamke mzinzi (13-18). Mialiko hii miwili imetenganishwa na mistari 6 inayohusu unyenyekevu (7-12).

Mialiko kutoka kwa wanawake hawa wawili inalingana sana: "Yeyote aliye wa kawaida, hebu aje hapa!" (4, 16). Wanawake wote wanafanya ombi sawa, lakini kila mmoja kwa sababu tofauti. Mmoja angependa kuwainua wanaohitaji hekima na kuwapa uhai, naye mwingine anataka kuwaelekeza kaburini wasio na ufahamu. Tambua kuwa wote wawili wana nyumba (1, 14) na wote wanatoa mkate (5, 17).

Wote wanazungumza (5-6, 17), lakini asili zao ni tofauti. Maneno ya Binti Hekima yanasikika wazi na vizuri kama kengele: "Kuwa mwenye busara." Maneno ya mwanamke mzinzi hunata na huchochea huku anashawishi kuwa "Maji ya kuiba ni matamu." Msomaji asiye na busara ana chaguo, lakini mwandishi amerahisisha maamuzi: njia hii inaelekea uzimani au mautini.

Mialiko hii miwili inayolingana lakini yenye ukinzani inaangazia mada kuu (7-12). Sehemu hii ya katikati inafafanua msingi wa kuchagua kwa busara— unyenyekevu! Soma mstari wa 7-12 kwa kuomba. Ukitii maneno haya utaishi. "Ukiyapuuza," mwandishi anaonya, "utajuta mwenyewe" (12).

Hii inatamatisha sura 9 zilizotangulia ambapo baba na Binti Hekima wanazungumza. Kwa kuhitimisha: Chagua uhai! Chagua hekima.

Andiko

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili