BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 14: Uovu na Maadili
Je, unakumbuka wanawake wawili katika sura ya 9, Binti Hekima na Mpumbavu? Tunakumbana nao tena katika sura ya 14. 14:1 inalingana sana na 9:1: Hekima huijenga nyumba yake na huishi kwa utakatifu, naye Mpumbavu huharibu na kugaagaa katika uchafu aliosababisha mwenyewe. Je, wanawake hawa wanalingana kwa chochote? Je, utachagua kumfuata yupi?
Sura ya 14 inatueleza na kutuonyesha tofauti kuu kati ya njia hizi mbili za maisha kwa kutumia sifa tofauti.
•Uangalifu au Kutojali (mstari wa 3,16)
•Ufahamu au Udanganyifu (mstari wa 8)
•Uadilifu au Dhihaka (mstari wa 9)
•Uangalifu au Haraka (mstari wa 15)
•Subira au Kughadhabika Haraka (mstari wa 29)
Soma tena orodha hii ya maadili na uovu. Ona jinsi mmoja hujenga, huku mwingine akiharibu.
Je, utachagua njia ipi maishani? Mstari wa 26 na 27 unasisitiza "kumcha Bwana," ambako humwelekeza mtu kwenye njia inayofaa. Kumcha huku sio woga, lakini ni heshima kuu inayochochea tabia njema hata wakati ambapo ni vigumu. Kumcha Mungu ni kuwa na ujasiri, ulinzi, uhai na wokovu.
Je, unadhani maisha yako yatakuaje ukimcha Mungu na kumchagua Binti Hekima?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili