Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Hekima ya MithaliMfano

BibleProject | Hekima ya Mithali

SIKU 16 YA 32

Sura ya 15: Hekima ya Mungu, Hekima Yako

Sura hii inataja sana jina la agano la kibinafsi la Mungu: Yahweh (linalotafsiriwa kuwa "BWANA" katika kiingereza). Limerudiwa mara 9 katika sura hii, na idadi hii inazidi mara ambazo limetajwa katika sura 5 zilizotangulia!

Kuna kitu cha muhimu kuhusu hilo. Katika sura ya 10-14 tulisikia mengi kuhusu maadili na tabia njema, lakini sasa yote yanahusishwa na uhusiano wetu wa kibinafsi na Mungu wa Biblia. Kitabu cha Mithali kwa kawaida hakihusu tu kuwa mtu mzuri, lakini mtu anayebadilishwa kupitia uhusiano wake na Yahweh.

Mafundisho muhimu katika sura hii yanajumuisha: mema yanayotokana na kuchuja maneno (mstari wa 1-4), umuhimu mkubwa wa kupata maelekezo (mstari wa 5-12), baraka inayotokana na furaha (mstari wa 13-18), siri ya mafanikio (mstari wa 19-24) na fadhila zinazotokana na moyo wa unyenyekevu (mstari wa 25-33). Ingawa hizi ni kanuni muhimu, hazina maana na faida yoyote ikiwa hazichochewi kupitia uhusiano na Mungu.

Unaposoma maudhui haya tofauti, angalia jinsi mwandishi anavyodokeza uhusiano na Yahweh unavyoingiliana na kanuni hizi za maisha. Je, mithali hizi zinaonyesha nini kuhusu Bwana? Je, kipi kinakuvutia zaidi?

Andiko

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili