BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Sura ya 17: Upatanifu na Kujizuia
Mithali ni nzuri sana! Tazama mstari wa kwanza katika sura hii kuhusu upatanifu majumbani: "Afadhali kula ukoko mkavu kwa amani na utulivu kuliko nyumba iliyojaa karamu na kuna ugomvi." Sulemani anaelewa--iwe wewe ni baba, mwana, ndugu, rafiki, mzee au kijana, upatanifu ni bora kuliko ugomvi.
Je, ni vipi ambavyo tunakuza upatanifu? Kwa kuwa upatanifu hutokana na kujizuia, mithali hii kwa kweli husisitiza kujidhibiti. Tazama mtiririko wa sura hii: mithali za kwanza 14 zinamalizia kwa taswira nzito kuhusu kujidhibiti ("Ugomvi ni kama kumwagika kwa maji, hivyo jiondoe kabla hayajamwagika"), nazo mithali zingine 14 zinamalizia kwa kuzungumzia kuhusu kuwa na tahadhari na unachonena. Tahadhari inayotolewa mwisho ni kuhusu maneno yetu. Maneno yanaweza kutuingiza kwenye matatizo, na Sulemani anatukumbusha kuwa tupunguze maneno.
Hekima nyingi katika sura hii imeelekezwa kwa mpumbavu, hasa mwana mpumbavu. Kulingana na Sura ya 17, inaonekana kuwa makao hayo ni mahali ambapo wapumbavu hujifundisha na kukua. Tuzifanye nyumba zetu kuwa maabara ya hekima! Unaposoma Sura ya 17, fikiria kuhusu nyumbani kwako na jinsi unavyoweza kuifanya kuwa mahali palipo na hali ya kujidhibiti
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili