BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 11: Hekima na Haki
Sura hii inaendelea kulenga "haki," neno la kibiblia linalomaanisha "uhusiano mwema." Mtu mwenye busara hujitahidi kutenda mema kwa wengine katika nyanja zote za maisha: uhusiano wa kibinafsi (5), majirani (9), raia wenzake (10-11), wafanyakazi wenzake (18), wanafamilia (21) na katika kumtumikia Mungu (30). Tambua jinsi mara kwa mara vitendo vya haki zinahusishwa na "ukombozi." Kinyume chake, waovu "wataanguka." "watashikwa mateka," "wataingia taabani," "wataangamia," na "wafe" Sura hii huyafanya maisha ya "uhusiano unaofaa" kuonekana ya kupendeza sana! Maana kimsingi, unaweza kuokoa maisha yako.
Ingawa kila mithali kwa kawaida hutumika pekee, wakati mwingine kuna vifungu ambavyo vinazungumzia wazo sawa. Katika sura ya 11 kuna mithali zinazozungumzia kuhusu kujidhibiti (12-13) na zingine kuhusu ukarimu (24-26) — dhana mbili zinazotofautiana. Tazama kwa makini kile ambacho tunapaswa kutoruhusu (kukejeli na umbea) ikilinganishwa na kile tunachopaswa kugawana (vitu vyetu). Tunapenda kutoa maoni yetu muhimu, lakini sio pesa zetu! Hekima ya kweli hufahamu wakati wa kufunga mdomo na wakati wa kufungua mikono.
Pia, tazama jinsi sura ya 11 inavyozungumzia kuhusu utajiri (4, 16, 28). Tunakumbushwa pesa sio muhimu kuliko vitu kama maisha, heshima na ustawi. Hata ukipata utajiri, usiweke imani yako kwake. Huhitaji pesa nyingi kuishi maisha mema.
Je, kuna mtu unahitaji kumwonyesha ukarimu leo? Je, kuna mtu unayepaswa kusita kumkashifu? Ruhusu sura hii ikuelekeze katika njia ya utakatifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili