BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
Sura ya 6: Usiwe Mpumbavu
Hotuba ya Tisa kutoka kwa Baba hadi kwenda kwa Mwana
Sura ya 6 ni hotuba ya tisa ya baba kwa mwanawe, na imejaa hekima. Unaposoma, tafuta maneno kama vile "mtego," "kushikwa," "mwindaji," "mwindaji ndege," "mporaji," "nasa," na "mwizi." Baba anasema, kuna wawindaji wanne wanaotaka kuivamia roho yako na kukunyang'anya maisha mazuri.
Jihadhari na:
Deni. (mstari wa 1-5)
Baba anamuonya mwanawe kuhusu hatari za madeni, hata ikiwa ni kumsaidia rafiki. Kukopa ni kama kujiingiza katika mtego. Usikope kwa jina lako, anasema. Ukikopa, jitahidi uwezavyo ulipe ("tia bidii kabisa") na ukimbie madeni kama vile swala au ndege (wanyama wawili ambao hukimbia kwa kasi sana).
Uvivu. (mstari wa 6-11)
Hapa baba anamwambia mwanawe kuwa "umaskini utamjia kama mwizi" asipofanya kazi kwa bidii. "Tazama sisimizi!" anasema, akionyesha jinsi wadudu hawa wana bidii ya kuhifadhi mavuno kwa siku zao zijazo. 1 Wafalme 4:33 inaonyesha Sulemani alikuwa mwana zuolojia na alijifunza mengi kutoka kwenye ulimwengu wa wanyama.
Umbea. (mstari wa12-19)
Katika mistari hii mada inabadilika kutoka kwa "mtu mvivu" hadi kwa mbea." Wote wanachukuliwa kuwa watu wasioheshimika, lakini baba anamkashifu zaidi mmbea. Mstari wa 16-19 unaoorodhesha mambo ambayo ni chukizo kwa Mungu, na mojawapo ni mtu anayesababisha mtafaruku wa kimahusiano.
Tamaa ya kimwili. (mstari wa 20-35)
Onyo hili la mwisho linachukua muundo wa hotuba. Tunakutana na mwanamke huyu mzinzi kwa mara nyingine. Mwanamke huyu atakuwinda, baba anasema na kushika mawindo yake kwa kope zake. Usidanganyike, kuingia kwenye mahusiano naye kutaleta uchungu tu. Yaani, baba anauliza swali, "Je, mtu anaweza kukanyaga makaa ya moto bila miguu yake kuchomeka?"
Maudhui kuu katika sura hii ni himizo la baba la kutahadhari wawindaji hawa wadanganyifu. Kujihusisha navyo ni kutupilia mbali uhuru na kujiletea majanga. Je, ni majaribu yapi yanayokuwinda leo? Yasalimishe kwa Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na ukumbuke kile alichosema baba: "kurekebishwa na kutii maagizo kunaleta uzima."
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili