Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Hekima ya MithaliMfano

BibleProject | Hekima ya Mithali

SIKU 4 YA 32

Sura ya 3: Ya Thamani kuliko Vito

Katika sura hii baba anamzungumzia tena mwanawe mara mbili, na lipo shairi kumhusu Binti Hekima.

Baba Anamzungumzia Mwanawe Mara ya Tatu

Mstari wa 1-12: Hotuba hii ni nzito na inajumuisha vifungu maarufu. Baba anaacha sisitizo la hapo awali kuhusu kuenea kwa maovu na anamhimiza mwanawe kushughulikia tabia yake mwenyewe. Chunguza matumizi ya maneno na jinsi baba anarudia neno "wewe/yako" kuonyesha matendo binafsi ya imani na matokeo yake.

Mpe Mungu kilicho bora zaidi ("Mazao yako ya kwanza") na utakuwa na utele ("maghala yako yatajaa na kufurika") Mistari miwili ya mwisho katika sehemu hii (11-12) ni tofauti kwa kuwa haiangazii manufaa ya kumheshimu Mungu. Badala yake, baba anamhimiza mwanawe kukubali nidhamu ya Mungu. Usiwe na uchungu mambo yakiwa magumu, anasema, ila amini kuwa Mungu huwakosoa Anaowapenda—kama baba kumwadhibu mwanawe.

Binti Hekima Anazungumza Mara ya Pili

Mstari wa 13-20: Hili ni shairi nzuri kuhusu hekima, na linamtumia tena mwanamke kama mhusika. "Ni wa thamani kuliko marijani; mwandishi anasema, "hakuna unachotamani kinachoweza kulinganishwa naye." Mshairi anamfafanua Binti Hekima kama mahali pa tulivu, mahali pa kupumzika na kiini cha amani—chenye uwezo. Analinganishwa na "mti wa uzima" kwenye kitabu cha Mwanzo 2:9, na katika mstari wa 19-20 tunaambiwa kuwa Mungu mwenyewe alitumia hekima kuumba ulimwengu: "Kwa hekima Mungu Aliiweka misingi ya dunia." Hekima ya Mungu ina uwezo mkuu katika ulimwengu huu na tunaweza kuipata!

Baba Anazungumza na Mwanawe Mara ya Nne

Mstari wa 21-35: Sura hii inaishia na hotuba nyingine kutoka kwa baba, akisisitiza tena kuwa njia ya hekima ni njia ya amani. Ukiwa mwenye hekima, utalala vyema, utaishi bila hofu na utajiepusha na mitego ambayo watu wengine huingia kwa urahisi. Baba anatoa ushauri kuhusu uhusiano unaolenga kuleta amani: lipa unachodaiwa, usiwadhuru watu, usiwashtaki watu bila ushahidi, na usitamani mali ambayo watu wanapata kupitia ukatili.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili