Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Mara nyingine Zekaria anaoneshwa hali ya watu wa Mungu. Wakati Yoshua alikuwa mwakilishi wao kwa upande wa kiroho, Zerubabeli yupo kama kiongozi kwa ajili ya ujenzi wa hekalu. Pia huduma yake inatendeka kwa kutegemea uweza wa Mungu na si vinginevyo. Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi (m.6). Kwa pamoja viongozi hao wawili wanapewa fursa ya kumtumikia Mungu katika ujenzi mpya wa taifa lake. Kupitia huduma yao taifa hilo litakuwa kama kinara cha taa kinachopeleka nuru ya Mungu duniani kote. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/