Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

SIKU 2 YA 31

Mfalme Daudializeeka mpaka ikawa ahitaji msaada wa kutunzwa kipekee. Inaonekana ilikuwepo desturi ya wazee wa umri na hadhi kama ya Daudi kutafutiwa wasichana kuwapatia joto la mwili. Abishagi, mshunami msichana mzuri, alionekana anafaa. Adonia alipoona hali ya baba yake, aliingiwa na tamaa ya kujinyakulia ufalme,akasema,Mimi nitakuwa mfalme(m.5). Sherehe aliyoifanya ilikuwa ya kiubaguzi. Hakuwakaribisha wale aliodhania watampinga: Sulemani nduguye, nabii Nathani, kuhani Sadoki, na Benaya jemadari wa vita.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/