Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Wayahudi walijua kutoka Maandiko Matakatifu kwamba Masihi atazaliwa katika ukoo wa Mfalme Daudi, ataitwa Mwana wa Daudi. Kwa hiyo walifikiri kwamba atafanana na mfalme Daudi, ingawa atakuwa mtawala mkubwa sana kuliko yeye. Yesu anawakumbusha kwamba pia Maandiko yasema kwamba Kristo ni Bwana wa Daudi, yaani, Mungu wake! Walishindwa kuelewa neno hili, kwa hiyo hawakumjibu Yesu. Yesu mwenyewe ndiye jibu! Ndiye mwana wa Daudi. Mama yake alikuwa nimwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu(1:27).Huyo [mtoto wa Mariamu] atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake(1:32).Munguametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu(1:69-70).Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi(2:4). Leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajile yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana (2:11). Mtu akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu (18:38).Vivyo hivyo Yesu ni Mwana wa Mungu.Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. ... Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu(1:31-32, 35).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/