Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Ufufuo wa mwili ni jambo la msingi katika imani ya Kikristo! Yesu alifufuka kimwili, kwa hiyo waumini wake pia watafufuliwa kimwili siku ile iliyopangwa na Mungu.Sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja(1 Kor 15:20-23). Leo Yesu analisisitiza jambo hili. Ila maisha ya ulimwengu ujao yatakuwa tofauti na maisha ya sasa. Hakutakuwa na mauti tena, tutaishi milele! Kwa namna hii tutafanana na malaika. Kwa hiyo hakutakuwa na haja ya kuzaa watoto kwa ajili ya kudumisha ukoo (swali katika m.31-33 linaonyesha kuwa waliouliza hawajaelewa sawasawa.Hata wa tatu akamwoa, na kadhalika wote saba, wakafa, wasiache watoto. Mwisho akafa yule mke naye. Basi, katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba). Hakutakuwa na hali ya kuoa na kuolewa kama ilivyo sasa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/