Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao(m.19). ”Waandishi” ni wataalamu wa Neno la Mungu (watheolojia). ”Wakuu wa makuhani” ni viongozi wa dini, ni wenyeviti wa baraza kuu la Wayahudi (maaskofu). Wao ni ”waashi” na Yesu ni ”jiwe kuu la pembeni” (m.17,Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni). Hawakutambua au hawakutaka kutambua ukuu wa Yesu, kwa hiyo wako hatarini sana, kama Yesu anavyoeleza katika m.18:Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; na ye yote ambaye litamwangukia litamsaga kabisa! Kwa maneno yake, Yesu amewaambia ukweli bila kuficha. Lakini badala ya kutubu wanazidi kuifanya migumu mioyo yao. Kwa ufahamu zaidi zingatia Ebr 3:12-15: Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/