Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Maombolezo ya m.12-18 hutuonyesha mtu mwenye mateso makali mno (ni vizuri kuirudia). Baada ya kutoa maneno yake ya dhiki akaanza kumwomba Bwana amwokoe. Hatimaye akapata uhakika kuwa Bwana amemsikia m.19-21 akasema,Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa. Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu. Kwa kunena zaburi hii akiwa msalabani, bila shaka Yesu alitaka kutuambia kuwa ndivyo mateso yake yalivyokuwa.Wamenizua mikono na miguu(m.16). “Kuzua” ni kutoboa. Yesu alisulibishwa kwa kupigwa misumari mikubwa katika miguu na mikono. Inaonekana katika anavyowaambia wanafunzi wake baada ya kufufuka:Akawaonyesha mikono yake na ubavu wake(Yn 20:20). Linganisha m.15 na Yn 19:28:Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti....Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu). Aliteswa kwa ajili yetu,alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona(Isa 53:5)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/