Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Kwa miaka yote zaburi hii imekuwa na nafasi ya pekee katika kanisa. Ni kwa sababu Yesu msalabani alisema maneno ya m.1:Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?Zaidi ya hayo, maneno mengine ya zaburi yanafanana sana na matukio yaliyotokea Yesu alipokufa msalabani. K.mf. linganisha m.6-8 na Mt 27:37-46:Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu. Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao; Husema, Umtegemee Bwana; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. ...Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI. Wakati uo huo wanyang'anyi wawili wakasulibiwa pamoja naye, mmoja mkono wake wa kuume, na mmoja mkono wake wa kushoto. Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema, Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani. Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu. Pia wale wanyang'anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile. Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?Hatujui ni tukio gani lililomfanya Daudi atunge zaburi hii, lakini ina maombolezo mengi. Alikuwa katika hali ngumu yenye mateso makali. Martin Luther alisema ni “zaburi ya mateso ya Kristo”.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/