Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Wakasimama mbali(m.12), maana mwenye ukoma alitengwa na watu. Alihesabika kuwa najisi kimwili na kiroho. Ukoma kwa Wayahudi ulikuwa mbaya kuliko magonjwa yote. Hapakuwa na tiba yoyote. Huenda walielewa Yesu ni tumaini lao la mwisho kupona. Tukijua haya yote tunaelewa mshangao wa Yesu anapouliza:Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?Zingatia wokovu ni zaidi ya kupona kimwili. Wote walipona, ila ni mmoja tu aliyeokoka, kama Yesu anavyosema katika m.19:Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/