Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Je, Yesu alipendelea kushirikiana na watu gani? Je, alipenda kujijenga kwa wenye vyeo katika nchi ili aishi katika majumba yao na kustarehe? Hapana! Yeyote aliyependa kumsikiliza na kupokea msaada wake ndiye aliyependa kukaa naye. Yesuakasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya(Lk 8:21). Hakujali uso wala cheo au mavazi ya mtu. Hakuwa na upendeleo. Yesu alimjibu na kumsaidia yule kipofu kama vile alivyofanya na yule mtu mkubwa katika somo la jana. Ndugu msomaji, umwite tu Yesu Kristo kwa ujasiri. Anakujali sana. Una thamani kubwa kwake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/