Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

SIKU 19 YA 31

Huyo mtoza ushuru ni kama mtoto mdogo mbele ya Mungu (ling. m.17,Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe). Hajisifu kwa lolote mbele ya Mungu, wala hadai chochote. Anajua kwamba kama yeye ataokolewa ni kwa neema tu. Akitambua kwamba hastahili, anajinyenyekeza mbele ya Mungu.Alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi(m.13).Kwa hiyo alipokea Ufalme wa Mungu siku ile, maana Yesu anasema katika m.17:Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe. Yeye asiyekuwa na haki alihesabiwa haki kwa neema ya Mungu. Yesu anathibitisha hiyo katika m.14:Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Dhambi ya Farisayo ni kwamba si mnyenyekevu mbele ya Mungu na anawadharau wengine. Katika m.9 wanatambulishwa kamawatu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote). Je, wewe unafanana na nani? Zingatia Mungu ni nani: Yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu (Isa 57:15).

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/