Sanaa Ya KustahimiliMfano
Rasilimali ya kuiomba
Fikiria uwe na hundi iliyo tupu itakayo kwa Mungu- ahadi ya hekima isiyo na mwisho.Unaweza kumuuliza ni wapi pa kuishi,jinsi gani ya kukabiliana na matatizo ya afya,jinsi gani ya kukabiliana na tatizo la kupoteza kazi ,au jinsi utakavyoweza kuishi siku ya leo.
Lakini kuna sharti moja.Ni lazima ujitoe kwanza kufuata hekima anayoitoa.
Maandiko ya leo tunayosoma yanatuambia ya kuwa kuna sehemu mbili katika sharti hili:
- Lazima “uamini”— lazima uje kwake kwa imani.Hii inaashirian ombi la uhakika.Ina maana kumtumaini Yeye,ukiwa na ujasiri katika tabia zake na Neno,na kujituma kikamilifu kufanya kile anacho kuonyehsa kukifanya.
- ”Haupaswi “kuwa na mashaka”—Haupaswi kuchukulia hekima ya Mungu kama vile ni Habari tu ya kuifikiria.Lazima ukubali kwa imani na usijaribu kuachagua kile unacho taka kukitii. Hii inamfanya mtu awe. wa nia mbili.Maombi ya namna hii ni yale ambayo mtu husema “tutaona.”
Tunapokuwa chini kabisa,katika hali ya kuwa na uhitaji sana,pasipo kuwa na popote pale pa kugeukial,Mungu ameahidi rasilimali yenye hekima ya ajabu sana.Atatuonyesha kile ambacho tunapaswa kukifanya,jinsi ya kufanya,na wakati wa kufanya,na ni nani wakufanya nae jambo hilo—kama mioyo yetu ikiwa wazi kumsikia Yeye na kujitoa kikamilifu kufanya kile anachosema.Inawezekana kabisa kuwa ,hekima yake siyo kitu tunachotaka kusikia.Lakini kama tukijitoa kufuatilia ,atatupa kwa ukarimu.
Today, accept the resource the Lord offers. Ask Him for wisdom and keep your eyes, ears, and heart open. You’ll see how He comes through.
Pokea rasilimali hii leo,ambayo Mungu anakupa.Muobe Yeye akupe hekimanna uweke macho,masikio,na moyo wako wazi.Utaona jinsi ambavyo atakujilia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maisha katika dunia hii yamejawa na majaribu .Yawezekana uko katikati ya moja ya majaribu hayo hivi sasa na ukiuliza, “kwa nini “? Au hata ,kuuliza “Nitaishije katika mapito haya? Kitabu cha Yakobo kina majibu! Katika mpango huu wa kusoma kwa siku tano,Chip Ingram anatuonyesha jinsi gani unaweza kuiona furaha ya Mungu katikati ya nyakati ngumu kwa kutumia ustadi kupitia Sanaa ya Kustahimili.
More
Tungependa kuwashukuru Wanaoishi Ukingoni kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://livingontheedge.org/product/art-of-survival-book/