Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Sanaa Ya KustahimiliMfano

Sanaa Ya Kustahimili

SIKU 2 YA 5

Tabia ya kuikumbatia

Mfungwa wa vita aliyestahimili miaka tisa migumu ya utumwa.Baada ya kuwekwa huru,mtu moja akauliza,je uliwezaje kuhimili, wakati baadhi ya marafiki zake hawakuweza. Alijibu bila ya kusita.Wale waliokuwa wakitarajia kuachiliwa mapema mara zote walikatishwa tamaa.Wakavunjika moyo,wakapoteza tumaini,na kupoteza Maisha yao.

Wahalisia waliojitoa kuvumilia walikuwa wamejiandaa kiakili kwa ajili ya magumu.Wale walio na matumaini,matarajio yao yaliposhindwa kutimia mwaka hadi mwaka,

”leo “wamepoteza mtazamo wao na wakashindwa kudumu”

Hakuna tatitizo lolote unapokuwa mtu mwenye matumaini!Bibilia inatuita kuishi katika matumaini. Lakini hatukuitwa kuishi tukiwa na matarajio yasiyo ya kweli(halisi) ya kwamba kila kitu kitakwenda vizuri.

Yakobo anasema kujaribiwa kwa imani kunaboresha mtazamo wetu kuhusu Mung una huleta saburi.Kama vile misuli ya wale wanaonyanyua vyuma katika mazoezi inyogawanyika kwenye mwili na ni kwa ajili ya kukuwa na kuwa na nguvu Zaidi wakijiandaa kwa msimu ujao,ndivyo ambavyo imani yetu inakuwa kila mara tunapokuwa tunastahimili jambo fulani.Ila hili ndilo linalojenga uvumilivu.

Haya ni maswali matatu ambayo yanawez kutusaidia kuwa na tabia ya uvumilivu.

Swali la 1: Ni jambo gani naweza kulidhibiti wakati dunia yangu inaposambaratika?

A1:Unaweza kudhibiti mtazamo wako,Katikati ya nyakati ngumu,unawezakuchagua furaha kwa sababu ya wema wa Mung na neema yake.Usichangaye mtazamo na hisia;maana unawezausijisikiekuwa na furaha.Ila kata kukata tamaa

Swali la 2: Nifanye nini ili niweze kuvuka siku ya leo?

A2:Lazima uvumilie.Tunapozidi kumtumaini Mungukwa uaminifu kabisa na kuzidi kudumu,ndivyo tunavyozidi kuwa na nguvu Zaidi.Dhiki zetu nyingi za leo huja kwa sababu ya kuwa na hofu ya kesho.Ila Mungu hajatuambia kujaribu kufikiria itakuwaje baabae.Badala yake inatupasa kutegemea neema ya Mungu ili tuweze kuvuka kila inapoitwa siku.

.

Swali la 3:Ni tumaini gani nililonalo kwa ajili ya kesho?

A3:Jibu lake ni,unalo tumaini lililo ndani ya Mungu kwa kujua yeye alivyo. Mungu ana vilivyo bora kabisa katika akili zake.Anaweza kutumia hali zilizo ngumu sana katika Maisha yetu,na kulitimiza kusudi lake kupitia hali hizo,na kuzigeuza kwa ajili ya faida yetu.

Leo hebu chukua mtazamo wa kuwa na furaha na imani.Kumbuka,nguvu ya Mungu hukamilika na kutimia katika madhaifu yako.Mbali na yale ambayo utayapitia mbeleni,utakuwa na neema ya kuyakabili.Mungu ataonekana.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Sanaa Ya Kustahimili

Maisha katika dunia hii yamejawa na majaribu .Yawezekana uko katikati ya moja ya majaribu hayo hivi sasa na ukiuliza, “kwa nini “? Au hata ,kuuliza “Nitaishije katika mapito haya? Kitabu cha Yakobo kina majibu! Katika mpango huu wa kusoma kwa siku tano,Chip Ingram anatuonyesha jinsi gani unaweza kuiona furaha ya Mungu katikati ya nyakati ngumu kwa kutumia ustadi kupitia Sanaa ya Kustahimili.

More

Tungependa kuwashukuru Wanaoishi Ukingoni kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://livingontheedge.org/product/art-of-survival-book/