Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 21 YA 31

Lugha inayotumika katika Ufunuo wa Yohana ni ya picha na mafumbo. Picha hizi zinawakilisha ujumbe mzito wenye maana iliyofichwa nyuma ya mafumbo. Viumbe wenye uhai wanne wanawakilisha sifa na tabia ya Mungu. Wana utukufu na uweza. Simba ni nguvu, ndama ni uaminifu, binadamu ni akili, na tai anawakilisha utawala (hali ya kuwa juu ya uumbaji wote). Pia nabii Ezekieli alionyeshwa picha hii, kama ilivyoandikwa katika Eze 1:5-10, Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu. Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana. Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi; mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele. Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng'ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia. Viumbe vyote vilivyoko mbinguni na duniani vipo kwa minajili ya kumtukuza Mungu. 

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/