Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 19 YA 31

Amasa alipoondolewa ... watu wote ... wakamwandama Yoabu ili kumfuatia Sheba (m.13). Hapa tunaona mfano wa ubishi wa Yoabu na kutokutii kwake. Alimwua Amasa ambaye Daudi alikuwa amemteua kuwa mkuu wa jeshi badala yake (19:13, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu). Yoabu aliona kuwa ili ufalme wa Daudi udumu, na taifa la Mungu lidumu, ni lazima yeye mwenyewe aendelee kuwa mkuu wa jeshi! Dalili ya Amasa kutokufaa ilishaonekana kwa jinsi alivyochelewa kufuata agizo la Daudi (m.4-6, Mfalme akamwambia Amasa, Uwakusanye pamoja kwangu kwa siku tatu watu wa Yuda, na uwepo wewe hapa. Amasa akaenda kuwakusanya Yuda; lakini akakawia zaidi ya huo muda aliowekewa. Basi Daudi akamwambia Abishai, Sasa Sheba, mwana wa Bikri, atatudhuru, kuliko Absalomu; twaa wewe watumishi wa bwana wako, ukamfuatie, asiingie katika miji yenye boma, na kujiponya machoni petu). M.22-23 inaonyesha kwamba Yoabu alikuwa mtu mwenye uwezo wa kutekeleza mipango. Alipokuwa amemshinda Sheba akamrudia mfalme na kuendelea kuwa mkuu wa jeshi.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/