Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 17 YA 31

Mimi naamua, Wewe na Siba mwigawanye hiyo nchi (m.29). Tukiangalia mambo yaliyotukia, hukumu hiyo ya Daudi haikuwa ya haki. Maana Siba, mtumwa wa Mefiboshethi, alikuwa amemdanganya bwana wake wakati Daudi alipokimbia. Alimsingizia kwa Daudi kuwa Mefiboshethi alitaka ufalme. Daudi alikuwa amemwamini, maana Mefiboshethi alikuwa ni mjukuu wa marehemu mfalme Sauli. Hivyo Daudi alikuwa amempa Siba mali yote ya Mefiboshithi. Daudi alipokipita punde hicho kilele cha mlima, tazama, Siba, mtumwa wa Mefiboshethi, akamkuta, na punda wawili waliotandikwa, na juu yao mikate mia mbili ya ngano, na vishada mia vya zabibu kavu, na matunda mia ya wakati wa hari, na kiriba cha divai. Mfalme akamwambia Siba, Ni za nini hizi? Siba akasema, Punda ni za jamaa ya mfalme wazipande; na mkate na matunda ni chakula cha hawa vijana; na divai ni kwamba wanywe hao wazimiao nyikani. Mfalme akasema, Na mwana wa bwana wako yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Angalia, anakaa Yerusalemu; kwani alisema, Leo nyumba ya Israeli watanirudishia ufalme wa baba yangu. Ndipo mfalme akamwambia Siba, Tazama, yote yaliyokuwa ni mali ya Mefiboshethi ni yako. Siba akasema, Mimi nasujudu; na nione kibali machoni pako, Ee bwana wangu, mfalme. (16:1-4). Haki ingalikuwa kwamba sasa Siba angaliyarudisha yote tena!



siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/