Kukua katika UpendoMfano
Upendo Unaokua Hung'aa Sana
Kwa heshima ya kusherehekea miaka 50 toka kutua mwezini, Harris Poll (kampuni ya utafiti wa masoko) ilichunguza watoto wa Marekani na kuwauliza watakapokuwa wakubwa wangependa kufanya nini. Kuwa nyota wa You Tube ilishika namba moja.
Kuliko hapo mwanzo, watu wanatafuta mwangaza wa utukufu binafsi. Kinyume chake, Wakristo wameitwa kuangaza kwa utukufu wa Mungu. Hiyo inaonekanaje kimatendo?
Hebu tuone kwa kuangazia baadhi ya vifungu vya maandiko ya siku ya leo.
… pata wokovu kwa matendo … kwa kuwa ni Mungu atendaye kazi ndani yako … Fanyeni kila jambo pasipo manung'uniko au mabishano, ili muwe wasio na mawaa na wasafi ... Ndipo mtakapong'aa… Wafilipi 2:12-15 SUV
… nuru yenu na ing'ae mbele za watu, ili waweze kuona matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu ... Mathayo 5:16 SUV
Msiwe wasikiaji tuu wa neno, na hivyo kujidanganya wenyewe. Fanya kama linavyosema. Yakobo 1:22 SUV
… Kinachohesabika ni imani ikijidhihirisha katika upendo. Wagalatia 5:6 SUV
Vifungu hivi vinaonesha kwamba mwanga wa Mkristo ni hatua ya kukua katika upendo kwa imani na ushirika na Roho Mtakatifu.
Kwa hiyo Mkristo anayeng'aa anafananaje? Ni mtu anayetabasamu wakati wote na haonekani kama kuna siku anakuwa na siku mbaya? Je, ni mtu ambaye anavutia kuwa mwema, au mtu unayemfahamu ambaye anaoneka ni mtoaji kwa nje?
Yawezekana, au haiwezekani. Kumbuka kwenda sawa na nafsi ya siku ya tatu--mtendo yetu na nia zetu ni muhimu.
Hebu chukua sekunde moja kufikiria juu ya nukuu hii bora kutoka katika kitabu maarufu Kijana, panya buku, mbweha na Farasi:
“Siyo ya kawaida. Tunaweza kujiona kwa nje tuu, lakini karibu kila kitu kinatokea ndani."
Upendo ung'aao huacha kuangalia juu juu. Haulinganishi, hauhukumu, haukosoi, na badala yake unamwangalia Mungu.
Tunang'aa upendo wa Mungu tunapojua vita vyetu ni juu ya giza la kiroho na kwa maombi tunapigania umoja na wafuasi wengine wa Kristo. Tunang'aa tunaposema na kutenda kinyume na dhuluma, kuishi kwa ukarimu na shukurani, kufanya mema yote tunayoweza, na kuwapenda adui zetu.
Tabia za kidunia zinajaribu kutuvuta katika kutafuta mapenzi yetu wenyewe, filosofia, umaarufu, na kusudi nje ya Mungu. Cha kushangaza, dunia imetengeneza ulimwengu wa watu ambao wamekua sugu kutokuwa salama na watupu. Aidha wamedharau au wamekataa kumtukuza na kumwinua Mungu.
Kinyume chake, watu wanaomtukuza Mungu sana wanajua utambulisho wao na umuhimu unatoka Kwake.
Ndugu na Dada katika Kristo, kuendelea kung'aa katika upendo wa Kristo, lazima tukumbuke kwamba tuko salama na wa maana kupitia kwa Kristo. Yeye ni maisha yetu, usalama wetu, na umuhimu wetu.
Na tunapoishi kwa Roho wake, kuwa salama jinsi tulivyo ndani yake, upendo ung'aao hutokea ndani yetu, na Mungu hupokea utukufu wote.
Oh, mtukuze Bwana pamoja nami, na tuliinue jina lake pamoja! Zaburi 34:3 SUV
Omba: Mungu wa upendo na nuru uliye mzuri na waajabu, nina nyenyekea mbele zako. Nitakutukuza wewe pekee. Ninakataa uongo wa kutokuwa salama. Wewe ni umuhimu wangu, na niko salama ndani yako. Nisaidie imani yangu ikue katika upendo ung'aao ulio safi na wa kujitoa. katika jina la Yesu, amen.
Pata zaidi kutoka kwa Mchungaji Pastor Amy katika vipindi vyake vya You’ve Heard It Said podcast.
Kuhusu Mpango huu
Kinachojalisha kwa kweli ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, lakini tunawapendaje kwa ufanisi? Ukweli ni kwamba, hatuwezi kuwapenda watu vizuri kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini tunapomuangalia Mungu na kunyenyekea, tunaweza kuishi katika nguvu kamili ya upendo wa Mungu. Jifunze zaidi kuhusu kukua katika upendo katika mpango wa siku 5 kutoka wa Mchungaji Amy Groeschel.
More