Kukua katika UpendoMfano
Upendo Unaokua Huwajali Wengine
Usifanye kitu chochote kwa sababu ya tamaa binafsi au kwa majivuno. Bali, katika unyenyekevu kuwathamini wengine kuliko wewe mwenyewe, siyo kwa kuangalia mapenzi yako mwenyewe bali kila mmoja wenu kwa mapenzi ya wengine Wafilipi 2:3-4 SUV (kuongeza msisitizo)
Upendo unaokuwa huwajali wengine. Siwezi kukupenda kweli kweli kama kila mara naangalia mambo yangu, ninachokikubali, tamaa yangu, au mafanikio yangu yajayo. Kwa hiyo kupendana, tunahitaji kuwa macho na mitego ya adui ambayo inatufanya tujiangalie wenyewe.
Nina amini kuvurugwa ni silaha ya msingi ya adui wetu wa kiroho. Adui yetu anataka kutuvuruga na nini? Jibu ni, kila kitu cha muhimu kwa Mungu. Kwa mfano:
- Kushiriki injili (Mpango wa Mungu wa kuokoa)
- Uhusiano wa karibu na Mungu
- Kupendana
Kweli, kama adui atatuvuruga kwa muda mrefu kwenye vitu hivi muhimu, anajua mgawanyiko, utengano, na uharibifu utatokea.
Kwanza, hebu tuainishe kuvuruga. Mwishowe, ni kila kitu kinachovuta hisia zetu au akili zetu kwenye kitu kingine. Na hapa kuna mifano ya kawaida ambayo inayoonesha kuvuruga: Una muda wa kupoteza wakati unasubiri miadi, na badala ya kumuomba Mungu kumhamasisha mtu unayeweza kumuombea, unaacha muda wako unapotea bure kwa sababu usikivu wako uko kwenye habari mpya, simu, mitandao ya kijamii, au aina fulani ya kutengwa burudani.
Nimekuwa hivyo, nimefanya! Ni tabia iliyo rahisi kuingia kwa sababu vyote vinapatikan vidoleni mwetu.
Lakini sitaki kuishi kwa kuvurugwa. Sitaki kuangukia kwenye tabia ya kubaki kama nilivyo. Sitaki kumpuuzia mtu aliye mbele yangu. Nataka kupenda kama Yesu!
Hebu na tuamke na ukweli kwamba hakika tunahitajiana. Kwa kweli, tafiti zinathibitisha kwamba jamii zenye afya zinazohusiana ni nzuri kwa ajili ya ustawi wa kimwili, kihisia na kisaikolojia.
Amua leo kuanzisha muunganiko wa makusudi na mahusiano ya mara kwa mara. Amua kuwa chanzo cha kumtia moyo yeyote unayekutana naye. Amua kuishi maisha yanayo fanana na upendo wa Mungu na kuangalia kusudi la Ufalme wetu.
Mume wangu, Craig, ni mtu anayenitia moyo linapokuja suala na kuishi maisha ya kuwajali wengine. Nimetengeneza orodha hapa ya jinsi mara zote namuona akiishi. Natumaini itakunia moyo pia:
- Mara nyingi hupiga simu kutaka kujua nani anaumwa.
- Ni mwaminifu kuwaombea watu.
- Hutumia muda kuelekeza au kusikiliza.
- Hufanya kinachotakiwa kufanywa--pasipo kujali gharama binafsi.
- Hutoa kipaumbele kwa familia na mimi.
- Hukiri na kuomba msamaha anapokosea.
- Hupanga njia za kuwa mkarimu.
- Mara zote hushukuru na hufurahi.
- Hujiweka wa mwisho.
- Siku zote humtia moyo mtu na kwa undani zaidi.
- Hukumbuka na hukiri siku muhimu ya msiba wa mtu.
- Huuliza maswali ya kufikirisha badala ya kuzungumza juu yake.
- Mara zote hula chakula na mtu kwenye sahani yake!
Maisha ya Craig’s yanaonesha tunda tamu lililoiva, la Roho Mtakatifu. Haya matendo yanayoonekana madogo lakini ya uaminifu ya upendo wa kujitoa ni ya mara kwa mara kwa sababu huchagua kuishi maisha ya Roho ndani yake. Kila siku, tunayo nafasi ya kufanya hivyo hivyo, kwa hiyo chukua muda kutafakari njia zozote unazoweza kuwapenda wengine.
Omba: Baba, fungua macho na mioyo yetu jinsi tunavyoweza kuishi maisha ya Kimungu, na kwa ajili ya wengine. Hasa hasa tusaidie kuweka mtazamo wetu kwa wale walio karibu nasi. Tuwapende kikweli na kuwathamini watu kwa matendo na maneno yetu. Katika jina la Yesu, amen.
Kuhusu Mpango huu
Kinachojalisha kwa kweli ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, lakini tunawapendaje kwa ufanisi? Ukweli ni kwamba, hatuwezi kuwapenda watu vizuri kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini tunapomuangalia Mungu na kunyenyekea, tunaweza kuishi katika nguvu kamili ya upendo wa Mungu. Jifunze zaidi kuhusu kukua katika upendo katika mpango wa siku 5 kutoka wa Mchungaji Amy Groeschel.
More