Kukua katika UpendoMfano
Upendo Unaokua Ni Mnyenyekevu
Unafurahia kujifunza ujuzi mpya? Nimekuwa najifunza kila siku masomo ya kihispania kwenye simu yangu kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Imekuwa muy divertido (ya kuchekesha sana)!
Ninapenda kukua katika maarifa na ufahamu kuhusu kila kitu. Ukweli, kuwa mjinga kuhusu jambo kunanitisha kidogo. Labda ni kwa sababu inanifanya nijisikiie katika mazingira magumu, mjinga, au siyo wa maana, wakati maarifa yananipa kujisikia jasiri.
Na sasa ni wakati wangu wa kukiri jambo ambalo ni baya kwako. Mimi ninapona kutoka mtu anayejua kila kitu, na napenda kuwa sahihi. Kama unaweza kuhusisha, natumaini masomo haya yatakubariki na kukusaidia!
Jambo ni hili: Kujifunza ni kuzuri. Hasa hasa tunatakiwa kukua katika ufahamu wetu wa neno la Mungu! Lakini kuna matatizo fulani na ufahamu, ambayo tutayaona katika maandiko ya leo.
Kwa kweli, nakutia moyo kutumia muda zaidi kusoma vifungu vya leo.
Unapofanya hivyo, kumbuka matatizo haya mawili ya ufahamu:
- Kwa urahisi tunaweza kutegemea ufahamu badala ya Mungu.
- Tunaweza kuwa wenye majivuno na watetezi wa ufahamu wetu.
Shauku hii ya ufahamu na kuwa sahihi hutengeneza jaribu kubwa kuwadharau wengine wanao fikiri au kutenda tofauti na wewe. Na kutukuza ufahamu kutakutenga mbali na wale wanaokosa mawazo yako.
Uko wapi basi upendo au nafasi ya kushuhudia injili katika mojawapo ya haya? Kama swali hilo linakuumiza kidogo, ujue kwamba ninajifunza hili pamoja na wewe!
Hatimaye, majivuno na upendo havikai pamoja.
Kupenda kama Yesu—ambaye, kama Mungu, alijua kila kitu na bado alijivua heshima yake ili kutumikia, kufundisha, na kuokoa wanadamu--tutahitaji kutembea katikaunyenyekevu wake.
Na kufanya hivi, lazima tupoteze kiburi chote.
Kupenda kwa unyenyekevu kama Yesu maana yake ni kueneza ufahamu wowote tulionao katika hekima na utambuzi wa Mungu. Hapo tuu ndipo tutakapoweza kwa huruma kushirikiana na watu, kuwauliza maswali, na kuwathamini kwa jinsi walivyo--katika furaha yao, au maumivu, katika dhambi au ujinga wao. Hivyo ndivyo Yesu alivyofanya.
Lazima tuwe W.K.K na watu: Wanyenyekevu. Kupenda. Kuwepo. Kwa sababu kuwapenda watu kunahitaji kuwaona na kuwasikiliza vizuri, siyo kuwaambia tuu.
Kila siku uchaguzi ni wetu. Tunaweza kuishi katika ufahamu wa kujihesabia haki, au tunaweza kuishi kwa unyenyekevu wa Yesu, neema ya ukweli na upendo uokoao.
Kama 1 Wakorintho 13 inavyotukumbusha, tunaona kwa sehemu tuu, lakini Mungu anaona picha yote. Kwa hiyo hebu tuamini njia yake ya upendo wa unyenyekevu.
Omba: Tulia na umtafute Baba. Muombe Roho Mtakatifu akufungue macho kuona kiburi chochote cha siri. Muombe akuhukumu kila mara kiburi kinapoinuka. Muombe upendo wa Mungu kuwa jambo linaloonekana sana kuhusu maisha yako.
Kuhusu Mpango huu
Kinachojalisha kwa kweli ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, lakini tunawapendaje kwa ufanisi? Ukweli ni kwamba, hatuwezi kuwapenda watu vizuri kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini tunapomuangalia Mungu na kunyenyekea, tunaweza kuishi katika nguvu kamili ya upendo wa Mungu. Jifunze zaidi kuhusu kukua katika upendo katika mpango wa siku 5 kutoka wa Mchungaji Amy Groeschel.
More