Kukua katika UpendoMfano
Upendo Unaokua Unahitaji Kwenda Sawa na Nafsi
Kupenda vizuri, tunahitaji kumaanisha, na nia njema. Kwa hiyo, upendo unaokua unahitaji kujitambua vizuri.
Upendo wako ni wa kumaanisha--ikimaanisha pasipo unafiki au maigizo? Fanya juhudi za makusudi kuweka nafsi yako sawa.
Mara nyingi nahitaji kwenda kwa wataalam wa viungo kwa ajili ya kurekebisha mgongo wangu. Bila shaka, Dk. Lisa siku zote anagundua kitu kilichohamisha usawa wa mgongo-- ndipo hunyoosha, hugonga, na kurudisha sehemu yake. Marekebisho hayo hufaidisha mwili wangu kwa njia tofauti.
Siku ya kwanza ya mpango huu wa Biblia, tulitambua kwamba tunahitaji sana msaada wa Mungu linapokuja suala la kumpenda Mungu kikamilifu na watu wengine. Na moja ya faida za kuziangalia kila siku na kumtegemea Mungu ni kwamba mara nyingi atakufunulia kitu maalum kinachohitaji marekebisho--au kwenda sawa na nafsi.
Mara nyingine, Mungu hunionesha kwamba ninalea kwa hisia za uoga badala ya upendo wa kweli, na ninahitaji kusalimisha hilo kwake. Mara nyingine, nakwazika, na Roho Mtakatifu ananionesha palipo na kiburi ili nitubu na kupata msamaha. Mara nyingi, nimejitegemea mwenyewe na kwa ubishi kutaka kuleta majibu kwenye mazingira ya juhudi za kusaidia kwa upendo.
Ninaweza kuendelea, lakini nachotumaini unaelewa nk kwamba hatuwezi kwa uhakika kupenda wengine mpaka tutakapokuwa tayari kupokea maonyo na kwa unyenyekevu kushuka chini mbele ya Daktari Mtakatifu.
Siwezi kupenda kwa hofu, chuki, ubinafsi, au ukaidi. Hata wewe huwezi. Hilo lizame ndani yako.
Tatizo ni kwamba vitu vingi ambavyo wewe na mimi tunafanya vinaweza kuwa na muonekano wa utakatifu. Sisi ni wazuri sana katika kujipendelea, kujihesabia utakatifu, na kujihesabia haki. Lakini upendo huzama ndani zaidi ya tunachokiona kwa macho.
Kitu chema siku zote si kitu cha upendo. Inapokuja kwenye upendo wa kweli, nia ni kitu cha muhimu zaidi.
Ndiyo maana tunahitaji kumwendea Mungu na mioyo ya unyenyekevu, iliyopondeka, kuondoa namna yoyote ya kujidanganya. Kama kwenda kwa daktari wa viungo, kuwa na muda wa makusudi na Mungu katika maombi kutaleta kujitambua nafsi zetu zinakokuhitaji.
Kwa hiyo leo, pata muda wa kujiuliza: Nimekuwa nafanya nini kinachoonekana ni sahihi, lakini kinakosa nia sahihi?
Omba: Muombe Mungu akuoneshe kama kuna nia mbaya unazohitaji kuziacha ili uweze kupenda kwa uaminifu.
Kuhusu Mpango huu
Kinachojalisha kwa kweli ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, lakini tunawapendaje kwa ufanisi? Ukweli ni kwamba, hatuwezi kuwapenda watu vizuri kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini tunapomuangalia Mungu na kunyenyekea, tunaweza kuishi katika nguvu kamili ya upendo wa Mungu. Jifunze zaidi kuhusu kukua katika upendo katika mpango wa siku 5 kutoka wa Mchungaji Amy Groeschel.
More