Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?Mfano
Maisha ya Kawaida Yameisha
Moto mtakatifu unaotoka kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu unakubadilisha kutoka kuwa mtu waw kawaida na kugeuka kuwa mtu mwenye uwezo na nguvu zaidi. Unachuka kazi au utumwa mtakatifu ambao unasababisha uishi maisha ya faida kwa wote, sio wewe binafsi pekee. Unatupilia uwoga na ubinafsi mbali na kutimiza lengo la Roho Mtakatifu. Unakuwa chombo kilichochaguliwa na Mungu.
Musa aliishi mahali ambapo aliona vichaka na miti kila siku kwa miaka arobaini. Hakuwa na tabia ya kuyasoma kwa makini au kuchunguza vichaka kwani vichaka vya porini havina maua ya kupendeza. Lakini, Mungu alichukua kichaka kimoja cha kawaida tu, na kutumia kichaka hiki kufanyia kazi ya ajabu. Alisababisha kichaka hiki kushika moto bila kuteketea (Kutoka 3:2) kisha, sauti yake Mungu ilitoka kutoka moto uliokuwa katika kichaka hiki. Musa, sawa na kichaka hiki, alikuwa mtu wa kawaida, isitoshe alikuwa mkimbizi aliyehukumiwa kwa mauaji, bila mipango kamili ya maisha yake. Alikuwa mchungaji na ‘maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.’ (Mwanzo 46:34)
Musa alishuhudia kichaka kikichomeka bila kuteketea. Hakuelewa kamili kwamba wakati huo ulikuwa chanzo cha mabadiliko katika maisha yake. Kwa udadasi, alichungulia tena na kustaajabishwa na kichaka hiki. Wakati huu, mwali mtakatifu uliruka kutoka moto wa kichaka na kuingia moyoni mwake. Musa, mtu wa kawaida, mkimbizi na muuaji, alibadilika, akawa Nabii. “Anawafanya malaika wake kuwa upepo, watumishi wake kuwa ndimi za moto.” (Waebrania 1:7) Siku itafika, wakati utajigeuza kustaajabu kichaka kinachochomeka, maisha yako yatabadilka kabisa.
“Uinjilishaji ni gari la moto lenye mjumbe anayeungua, akihubiri Injili inayowaka moto juu ya magurudumu ya moto! Ruhusu Roho Mtakatifu kuyafanya maisha yako kuwa gari lake. ” Reinhard Bonnke.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kuna nguvu ya kipekee, nguvu inayofufusha ndani yako. Mwinjilisti Reinhard Bonnke amekutolea maandishi ya nguvu kuhusu Roho Mtakatifu na Kanuni za Nguvu zake Roho Mtakatifu. Funzo hili la siku saba litapinga mawazo au fikra zako kuhusu Roho Mtakatifu na
More
Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en