Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?Mfano

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

SIKU 2 YA 7

Yesu alibatizwa katika Roho Mtakatifu.

Ingawa Yesu alizaliwa kutoka nguvu za Roho Mtakatifu, alihitaji kubatizwa katika Roho Mtakatifu alipokuwa akiaanza kazi ya Injili. Wakati Yohana Mbatizaji alipombatiza Yesu katika mto wa Yordani, kibatizo cha pili kilitendeka wakati Roho wa Mungu ulishuka kwake Yesu, kama njiwa, sio katika mfano wa ndimi za moto kwa sababu kulikosekana dhambi za ‘kuchomwa’ ndani yake Yesu.

Mtindo wa kipekee katika waKristo ni Yesu kwa kuwa alibatizwa katika Roho Mtakatifu. Vitabu vya Injili, yaani, Mathayo, Marko na Luka vyote vinatangaza habari hizi. Katika kitabu cha nne, Yohana, alifafanua habari hizi zaidi. Yohana Mbatizaji, aliyeaanza kazi ya uhubiri na utafsiri mbele yake Yesu alisema, (Yohana 1;32) ”Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. Yesu Kristo mwenyewe alifafanua, Luka 4:18, “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.”

Petero, katika kitabu cha Matendo ya Mitume 10:38 alisema, “Mnafahamu jinsi Mungu alivyompa Yesu wa Nazareti Roho Mtakatifu na uwezo, na jinsi alivyozunguka kila mahali akifanya mema na kuponya wote waliokuwa wakiteswa na nguvu za shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. Yohana Mbatizaji alinena jambo la kusisimua, “Mimi nisingemtambua, lakini Mungu ambaye alinituma nibatize watu kwa maji alikuwa ameniambia kwamba, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.” (Yohana 1:33)

Yesu Kristo alipata kupitia mitindo za kibinadamu ili Mungu aweze kuonyesha mfano wa ubinadamu bora. Alikuwa wa kwanza katika umati wa watu. Alikuwa mtu wa kwanza kupata ubatizo katika Roho Mtakatifu. Yohana 3:34 insema, “Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu kwa maana Mungu amempa Roho wake pasipo kipimo. Yohana 1:16 inasema, “ Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. Huu ni ukweli mwema – alichopokea Yesu ni chetu pia. Alijazwa na Roho Mtakatifu kwa ajili yetu, na katika kujazwa huku, sisi pia tunajazwa na Roho.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Kuna nguvu ya kipekee, nguvu inayofufusha ndani yako. Mwinjilisti Reinhard Bonnke amekutolea maandishi ya nguvu kuhusu Roho Mtakatifu na Kanuni za Nguvu zake Roho Mtakatifu. Funzo hili la siku saba litapinga mawazo au fikra zako kuhusu Roho Mtakatifu na

More

Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en