Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?Mfano
Moto wa Mwenyezi Mungu katika Yesu.
Kwa wengi, ilikuwa Hekalu la kumwabudu Mungu. Kwa wengine, ilikuwa soko la biashara, mahali walitoa riziki kwa njia yeyote iwezekanavyo. Lakini, kwake Mwana wa Mungu, Ilikuwa Jumba la Baba yake - Hekalu takatifu, mahali pa maombi na pa kupokea wokovu, mahali pa kuponywa na ukombozi wa mataifa. Kwa hivyo, hasira zilizomtoka na viboko vya kuwapiga waliopiga biashara, wezi, wahuni na watesaji. iliwakasirisha sana Wafarisao na kuweka maisha ya Yesu hatarini. Lakini, heshima zake Mungu baba yake zilkuwa zimetolewa na hizi dhambi na ukombozi wa mataifa ulikuwa katika vipimo. Yesu alichekelea kifo kwa sababu alijua ni fanaka kwa wote. Alikubali kuenda msalabani kama ingekuwa ni lazima aende. Shauku kubwa kweli!
Katika mitindo ya kibinadamu, moto wa mwenyezi Mungu unatafsiriwa kuwa shauku ya kipekee – aina ya shauku tunaona ikiwa ndani yake Yesu. Inawezekana kuwa, moto wake ulikuwa zaidi ya maneno au mafunzo yake. Wakati Yesu alisafiri Yerusalemu mara ya mwisho, tunasoma kwamba alitembea mbele ya wafuasi wake. Walipata kutazama jinsi alivyo jihimiza kuendelea mbele (Marko 10:32) Kwa nini? Kwa sababu moto uliokuwa ndani ya roho yake ulionekana jinsi alivyotembea.
Walipofika Yerusalemu, Yesu aliona uharibifu uliokuwa katika Hekalu Takatifu, Wafuasi wake walipata kushuhudia shauku au hasira za Yesu. Hasira zake Yesu zilimbadilisha kuwa kiumbe cha kustaajabisha. Wafuasi wake walikumbushwa maneno ya Zaburi 69:9 “Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.” Ilhali chanzo cha hasira zake Yesu zilitoka kwa upendo, sio hasira za ubaya au madharau. Yesu hakuwa mwenye ukali wa kupindukia. Alipenda sana Hekalu ya Baba yake. Alitaka sana kuwaona watu ndani ya Jumba hili, wakimwabudu Mungu wakiwa huru na kwa furaha. Lakini, hali ya kiuchumi au kibiashara katika Jumba la Mungu ilizambaratisha mtindo huu na kusababisha hasira zake kutoka. Moto wa Roho Mtakatifu ndani yake ulimhimiza kuwatorosha na kuisafisha Hekalu.
Watoto, vipofu na walemavu walibaki na kuponywa na Yesu, (Mathayo 21:14-16) “Vipofu na vilema wakamwendea, naye akawaponya. 15Lakini makuhani wakuu na walimu wa sheria waliudhika walipoona mambo ya ajabu aliyoyafanya na kuwasikia watoto wakishangilia Hekaluni wakisema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi!” Wakamwuliza Yesu, 16 “Unasikia hawa wanavyosema?” Akawajibu, “Nasikia. Kwani hamjasoma maneno haya, ‘Kutoka katika vinywa vya watoto wadogo na wale wanaonyonya umeleta sifa kamili’? ” Hili ndilo lilikuwa lengo lake mwanzoni na kusababisha hasira moto zaidi. Alifaulu kwani Watoto waliimba “Hosana!"
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kuna nguvu ya kipekee, nguvu inayofufusha ndani yako. Mwinjilisti Reinhard Bonnke amekutolea maandishi ya nguvu kuhusu Roho Mtakatifu na Kanuni za Nguvu zake Roho Mtakatifu. Funzo hili la siku saba litapinga mawazo au fikra zako kuhusu Roho Mtakatifu na
More
Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en