Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?Mfano

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

SIKU 6 YA 7

Ubatizo wako wa kwanza.

Umeumbwa, kuchaguliwa na kubatizwa na Mungu kwa ubinafsi wake, kutimiza matakwa yake kwa muda aliyekuchagulia. “Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.” (Kumbukumbu la Torati 33:25) Badala ya kuhangaishwa na kile usichonacho kwa sasa, tilia maanani yale uliobarikiwa kupata na kukanyaga nje kwa imani kamili ili upata kushihudia Mungu akikamilisha kazi zake kupitia kwako.

Katika siku ya Pentekoste, waumini 120 hawakulilia kibatizo cha Roho Mtakatifu mara ya pili. Tafadhali kumbuka, HAKUNA MMOJA WAO ALIYEKUWA KATIKA CHUMBA CHA JUU AMBAYE ALITOKA NA NDIMI MBILI ZA MOTO KICHWANI. “Pakatokea kitu kama ndimi za moto ambao uligawanyika ukakaa juu ya kila mmoja wao.” (Matendo ya Mitume 2:3) lakini, mwali huu unawakilisha au una maana ya Moto wa Mungu - Mamlaka, Nguvu na Utukufu.

Ninaposafiri kote duniani, wakati mwingi watu wananiuliza “tafadhali, niombee. Nigependa kupata uwezo au ubatizo wako.” Jibu au swali langu huwa, “Nikupa tuzo au ubatizo wangu, nitabakia bila uwezo wa Mungu? La hasha.” Lakini, pata siri ya furaha: Ukipata uwezo au ubatizo wa Reinhard Bonnke, utakuwa mfano wa Bonnke. Wacha nikueleze: Singependa kuwa mfano wa mtu mwingine na Mungu hataki uwe mfano wa binadamu mwingine.

Ukitaka kujua asili yake Mungu, tafakari mazingira yetu. Binadamu waliozidi millioni 7.5 wote wako na alama za vidole tofauti. Hakuna tawi la mti mmoja linalofanana na lingine. Mbona? Kwa sababu Mungu hafanyi kurudia alichoumba. Mungu ni Muumbaji hodari. Mungu anatoa hati au asili halisi bila kurudia. Mwali ulioko kichwani chako ni cha kibinafsi, linalo jina lako. Mwali huo ulitengenezwa kuwa wako pekee. Hauwezi kutumiwa na mtu mwingine. Hakuna mtu duniani anayeweza kumtumikia Mungu kama wewe! Wewe ni kiumbe cha kipekee na pia, ubatizo au upako wako ni wa kipekee.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

Kuna nguvu ya kipekee, nguvu inayofufusha ndani yako. Mwinjilisti Reinhard Bonnke amekutolea maandishi ya nguvu kuhusu Roho Mtakatifu na Kanuni za Nguvu zake Roho Mtakatifu. Funzo hili la siku saba litapinga mawazo au fikra zako kuhusu Roho Mtakatifu na

More

Tungependa kumshukuru CfaN Christ Kwa Mataifa Yote kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://cfan.org/?office=za&language=en