Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 18 YA 31

Waisraeli walifukuzwa katika nchi yao kwa sababu ya dhambi. Mataifa yakashiriki kumtukana Mungu kuwa ni dhaifu mbele za miungu yao. Sasa Mungu atasahihisha mawazo hayo ya kinyume. Atawarudisha watu wake katika nchi yao, na kuwatakasa na uchafu wa zinaa ya kiroho. Hivyo wataongozwa na Roho wa Mungu wakiwa na moyo mpya ulio tayari kutimiza mapenzi ya Mungu. Mungu hufanya haya yote kwa ajili ya jina lake takatifu, yaani, si haki ya Waisraeli. Ni kwa neema tu. Linganisha m.22 na Tit 3:4-5, Waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaendea  ↔  Wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu k...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha