Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Mungu ni Mweza, hakuna linaloshindikana kwake. Uweza wake hudhihirika kwa neno na matendo yake. Ezekieli anaambiwa kuwa yeye Mungu atafanya jambo lisilowezekana: Atahuisha taifa la Israeli, ingawa hufanana na kukusanya mifupa mikavu iliyotawanyika, kuiunganisha, kuotesha mishipa, nyama na ngozi, na hatimaye kupuliza uhai ndani yake. Ni mfano unaoonyesha kuhuishwa kwa Israeli – na hata kwetu. Jambo gumu la kupata uhai mpya linawezekana kwa Mungu. Hakika hakuna jambo la kumshinda Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz