Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 16 YA 31

Sote tumeitwa kutenda haki na huruma. Lakini Waedomu walifanya tofauti. Ni ndugu wa Waisraeli, wote wakiwa watoto wa Isaka. Na Waedomu walikula njama na Waisraeli dhidi ya mfalme wa Babeli (Yer 27:3, Jifanyizie vifungo na nira, ukajivike shingoni; kisha uvipeleke kwa mfalme wa Edomu, na mfalme wa Moabu, na mfalme wa wana wa Amoni, na mfalme wa Tiro, na mfalme wa Sidoni, kwa mikono ya wajumbe watakaofika Yerusalemu kwa Sedekia, mfalme wa Yuda). Lakini baadaye, Wababeli walipoangamiza Yerusalemu, Waedomu waliwatoa tu ndugu zao, tena kwa lengo baya la kumiliki nchi yao. Walijua ni kushindana na Mungu wa agano na Israeli (taz. m.10, Umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa Bwana alikuwako huko), hata hivyo walifanya! Hukumu ya Mungu juu ya Edomu itukumbushe kutoiga mfano wao mbaya.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu k...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha