Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 23 YA 31

Tunakumbushwa kutimia kwa ahadi ya Mungu ya kuleta Msaidizi atakayewaongoza waumini. Roho Mtakatifu aliposhuka, waumini wote waliokuwapo walianza kusema kwa lugha mpya wakimsifu Mungu. Watu waliosikia walidhihaki kwanza, lakini Petro alipowaelezea maana yake, wakachomwa mioyo yao, wakatubu, wakapokea aliyowaambia. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu (m.41), ambao pamoja na kubatizwa walimpokea Roho Mtakatifu. Hata sisi leo ni vema tutubu makosa yetu na kuiamini Injili. Roho Mtakatifu yupo kwetu leo. Tumkaribishe kwa njia hiyo hiyo, yaani kwa kuipokea Injili na kubatizwa, ili akae mioyoni mwetu, na siku ya mwisho tuurithi uzima wa milele.

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz