Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 22 YA 31

Somo linaeleza makkundi mawili ya watu. Kundi la kwanza wameitwaje? Ni watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya (m.14). Hawa, tumaini lao lote li katika maisha haya; wamejibidisha kutafuta utajiri na anasa za dunia hii. Huwawekea wototo wao hazina za mali ya ulimwengu huu – basi! Kundi la pili ni la wamtumainio Mungu. Hawa hufanya nini? Mtunga zaburi anajibu katika m.4-5, akimwambia Mungu, Kwa neno la midomo yako nimejiepusha na njia za wenye jeuri. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, hatua zangu hazikuondoshwa. Anafanya hivyo, akiendelea kumwomba Mungu, Nikutazame uso wako katika haki, niamkapo nishibishwe kwa sura yako (m.15). Hayo ni jumlisho la yote wayafanyayo na wanayoyatamani. Hatari nyingi zawazunguka, lakini Mungu amekuwa kimbilio lao. Hakikisha kundi lako leo. Chagua kundi la pili, ukilifanya ombi la mtunga zaburi kuwa ombi lako! 

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz