Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 11 YA 31

Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu (m.11). Yesu alitumia sana mifano alipowaeleza watu juu ya ufalme wa Mungu (m.2, Akawafundisha mambo mengi kwa mifano). Hivyo aliiweka wazi habari ya ufalme wa Mungu, haikuwa tena siri. Hata hivyo kuna wengine waliokuwa hawaelewi. Ila wanafunzi wa Yesu walitambua, maana walipokea kwa imani (m.20, Hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea). Ndivyo ilivyo hata leo! Fundisho: 1. Neno la Yesu lipewe umuhimu wa kwanza kwa maisha yetu yote. 2. Tumsihi Yesu atufunulie maana ya neno lake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Tufanye kama wale Thenashara, walimwuliza habari za ile mifano (m.10).

Andiko

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha